• Home
  • Kongamano la kwanza la kamisheni ya kiswahili Afrika Mashariki

Kongamano la kwanza la kamisheni ya kiswahili Afrika Mashariki

Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania imesema itahakikisha lugha ya kiswahili inaendelea kutumiwa ipasavyo kwa Nchi wanachama wa jumuia ya Africa mashariki.

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la Kwanza la kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki Mjini Zanzibar Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassani amesema lugha ya kiswahili ni lugha ya mawasiliano hivyo ni vyema kuendelea kutumiwa katika nchi za Africa Mashariki.

Amesema ni jambo la busara kwa jumuiya ya Afrika mashariki kuamua kuanzisha kamisheni hiyo visiwani Zanzibar ukizingatia ndio sehemu ya chimbuko la lugha hiyo.

Aidha ametowa wito kwa kamisheni hiyo kuendeleza mikakati zaidi ikiwemo kuendelea kuwakutanisha pamoja wadau wa lugha ya Kiswahili kwa lengo la kuikuza na kuieneza lugha hiyo ndani na nnje ya nchi.

Kwa upande wake Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo Zanzibar,Rashid Ali Juma alisema Serikali ya mapinduzi Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano kwa kamisheni hiyo kuwepo hapa Zanzibar kutokana na Zanzibar kuwa ni sehemu ya chimbuko la lugha hiyo.

Nae Kaimu mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika mashariki Balozi Agostino Mahiga alisema kutokana na mataifa mbalimbali kuwa na mwamko wa kutumia lugha ya Kiswahili hivyo wananchi wanajukumu kubwa la kuitunza na kuendeleza kuitumia lugha hiyo ili iweze kueneo kwa urahisi katika nchi mbalimbali.

Kwa upande wake katibu mtendaji wa kamisheni ya Kiswahili Prof.Kenneth Samala amesema wanaendeleza mashirikiano na serikali pamoja na taasisi zote kwa lengo la kuimarisha lugha ya kiswahili dunia kote.

Kongamano la kwanza la kamisheni ya kishwahili jumuiya ya Afrika mashariki litaendelea kufanyika Zanzibar kwa muda wa siku mbili ambapo limeshirikisha jumla ya washiriki 150 kutoka nchi tofauti za Africa ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Sudani kusini, Rwanda, na Burundi.

Na: Fat hiya Shehe   |  Zanzibar24

Leave a comment


East African Kiswahili Commission
Maisara Street
P.O. Box 600
Zanzibar, Tanzania
Tel: +255 024 2232704/
+255 024  2232722
katibumtendaji@kiswacom.org
katibu.tume@kiswacom.org